MADAKTARI NCHINI UINGEREZA WATOA TAHADHARI JUU YA UGINJWA MPYA WA MAPAFU NCHINI MWAO

Madaktari nchini Uingereza wametoa tahadhari kuhusu virusi vipya vya mapafu ambavyo vina uwezo wa kuua.

Mwanaume mmoja kutoka nchini Qatar, anatibiwa mjini London baada ya kuambukizwa virusi hivyo akiwa Mashariki ya kati.
Virusi hivyo ni sawa na vile vya SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) vyenye makali mno na ambavyo vilisababisha vifo vya mamia ya watu barani Asia mwaka 2003.
Hiki ni kisa cha pili cha maambukizi ya virusi hivyo vipya vijulikanavyo kama (coronavirus) kuthibitishwa.
Viligunduliwa mwanzo kwa mgonjwa nchini Saudi Arabia, ambaye inasemekana alifariki baadaye.

Comments