
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI:
Release No. 144
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 13, 2012
KAMATI YA UTENDAJI YAREKEBISHA KANUNI
Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba
12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam imepitisha marekebisho ya kanuni kwa
ajili ya Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.
Marekebisho hayo
yametokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano uliofuta Ligi ya Taifa.
Hivi sasa kutakuwa na Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Mkoa na
Ligi ya Wilaya.
Kutokana na
marekebisho hayo ya kanuni; Ligi ya Wilaya itaendeshwa na Vyama vya
Mpira wa Miguu vya Wilaya (DFAs), Ligi ya Mkoa itaendeshwa na Vyama vya
Mpira wa Miguu vya Mikoa (RFAs).
Mechi za mchujo (play
offs) kutafuta timu zitakazopanda kwenda Ligi ya Mkoa zitaendeshwa na
RFAs wakati play offs za kupanda Ligi Daraja la Kwanza zitakazohusisha
mabingwa wa mikoa zitasimamiwa na TFF.
Ligi za madaraja yote zitachezwa mwaka mzima kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
TFF KUTOA VIFAA VYA MIL 7/- HOSPITALI YA TEMEKE
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) litatoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 7.3
kwa Hospitali ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambazo ni asilimia 5 ya
fedha zilizopatikana kwenye mechi ya Simba na Azam.
Mechi hiyo ya Ngao ya
Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2012/2013
ilichezwa juzi (Septemba 11 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kuingiza sh. 146, 640,000. Washabiki 26,001 walikata tiketi kushuhudia
mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-2.
Sekretarieti ya TFF
inatarajia kukutana na uongozi wa Hospitali ya Temeke wakati wowote
kuanzia leo ili kujua mahitaji halisi kabla ya kufanya ununuzi wa vifaa
husika.
Mgawanyo wa mapato ya
mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) sh. 22,368,813.56, asilimia 5 ya mchango wa kusaidia jamii
(Hospitali ya Temeke) sh. 7,332,000, uwanja sh. 10,148,318.64, Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 4,059,327.46, TFF
sh. 10,148,318.46 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
5,074,159.32.
Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) sh. 1,014,831.86, kila timu sh. 32,265,025.93, asilimia 10
ya gharama za mchezo sh. 10,148,318.64, nauli kwa waamuzi na kamishna
sh. 80,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi na kamishna 230,000, posho ya
waamuzi 400,000, tiketi sh. 4,495,800, maandalizi ya uwanja (pitch) sh.
400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi uwanjani sh. 2.350,000 na
Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000.000.
Mchango wa kusaidia
jamii kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuzindua msimu uliopita kati ya
Yanga na Simba ulikuwa sh. 15,000,000 ambazo zilikwenda Chama cha
Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kusaidia uchunguzi wa kansa ya
matiti kwa akina mama.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments
Post a Comment