Skip to main content
KUNDI LA M23 LAKANUSHA TUHUMA KATIKA REPORT YA HUMAN RIGHT KUHUSU KUTEKELEZA MAUAJI YA KIVITA
Kundi la
Waasi la M23 linalopambana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo DRC Mashariki mwa Taifa hilo limetuhumiwa kuhusika na mauaji ya
raia sambamba na makosa ya kivita katika ripoti iliotolewa na Shirika la
kimatiafa linalo tetea Haki za Binadamu "Human Rights Watch"
.Shirika la Kutetea Haki za BinadamuHuman Rights Watch limesema
Kundi la M23 limeendelea kutekeleza mauaji ya watu wasio na hatia pamoja
na kuendelea kuajiri watoto wadogo na kuwauwa vijana wanaopinga
kujiunga na kundi hilo, vitu ambavyo vinakwenda kinyume na sheria za
kimataifa.Kwa mujibu wa Anneke Van Woundenberg wa Human Rights Watch tawi la
Afrika amesema ripoti hiyo imetolewa baada ya uchunguzi wa kina
uliofanyika kati ya mwezi Mei na Septemba mwaka huu ambapo takriban watu
zaidi ya 190 walihojiwa.Miongoni mwa watu waliohojiwa katika uchunguzi huo ni pamoja na
waathirika wa vita hivyo raia wa Congo na wa Rwanda, wajumbe wa familia
za waathirika, mashahidi, viongozi mbalimbali wa vijiji pamoja na
wapiganaji zamani wa kundi la M23.Anneke Van Woundenberg amesema hata viongozi wa Rwanda wanaweza
kuchukuliwa kama washirika wa mauaji hayo kwa kuwapa msaada wa kijeshi
wapiganaji wa kundi la M23. Jambo ambalo vingozi wa Rwanda wanaendelea
kukanushaKiongozi huyo wa Human Rights Watch tawi la Afrika amesema kwamba ni
muhimu kwa kipindi hiki wafadhili wa Rwanda kuchunguza mdaada unaopewa
kwa nchi hiyo iwapo hauchangii kuchochea machafuko mashariki mwa
DRCongo.Mwenyekiti wa kundi la M23 Jean Marie Runiga ametupilia mbali tuhuma
hizo huku akisisitiza kuwa M23 haijawahi kupewa msaada wowote kutoka
ugenini, na kwamba hawajawahi kutekeleza mauaji yoyote, vijana
wanaoajiriwa katika kundi hilo wanakuja kwa khiari yao, na iwapo kuna
mpigananii wa M23 ataehusika na tukio hilo atahukumiwa kwa mujibu wa
sheria.
mh
ReplyDelete