Skip to main content
KENYA YAPATA MASHAMBULIZI YA KULIPIZWA KISASI
Takriban watu kumi na moja wa kabila la Pokomo wameuawa katika
mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi katika eneo la Tana River,Kusini
Mashariki mwa Kenya.Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema alisikia watu wakipiga
mayowe wakati kijiji kimoja kilipokuwa kinashambuliwa na kisha wenyeji
kuteketezwa.
Eneo hilo ambalo kunaishi jamii za kuhamahama ni kitovu cha mizozo ya ardhi na maji kati ya jamii za Orma na Pokomo.
Watu wengine kumi walijeruhiwa kwenye uvamizi huo uliotokea asubuhi ya kuamkia leo.
Uvamizi huu umetokea baada ya mashambulizi
mengine kutokea mwezi jana ambapo watu 52 kutoka jamii ya Orma wengi
wakiwa watoto na wanawake kuuawa kwa kunyongwa na kuteketezwa kiasi cha
kutotambulika.
Ni katika tukio ambalo lilitajwa kuwa ghasia
mbaya za kikabila kutokea katika miaka ya hivi karibuni nchini Kenya.
Polisi na viongozi wa kijamii walisaidia kutuliza hali na kurejesha
usalama kati ya jamii hizo mbili.
Ingawa hali ya wasiwasi ilisalia kukumba eneo hilo.
Jamii hizo mbili za Pokomo na Orma, zimekuwa zikizozana kuhusu matumizi ya ardhi na maji ambazo ni rasilimali adimu.
Wapokomo ni wakulima ambao hukuza chakula kando ya mto Tana wakati jamii ya Orma ni wafugaji wa kuhamahama.
Comments
Post a Comment