Skip to main content
KAMA UNATATIZO LA KUKOSA USINGIZI HII INAKUHUSU. JUA SABABU NA MATIBABU PIA
Tatizo la kukosa usingizi huenda
likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya sahau au ''Alzheimer'' kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana maumbile
yanayofananishwa na binadamu.
Vipande vya protini, kwa lugha ya kitaalamu
(plaques) au uchafu kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti
inayosababisha maradhi haya.
Utafiti uliofanywa na kuchapishwa
katika jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde
chembe chembe za uchafu ule ulipoanza kukua kwenye ubongo wa panya,
usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao.
Taasisi inayosimamia utafiti wa maradhi hayo,
(Alzheimer's Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza
kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari.
Utafiti wa kutaka kugundua mapema kama mtu
anaelekea kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika
kutibu maradhi hayo.
Wagonjwa hawaonyeshi dalili kupitia hisia au
kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa.
Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi kwamba tiba
inakua vigumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.
Ndiyo sababu wataalamu wanafanya juhudi za
kuanza mapema kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa kabla
ya dalili hizo kujitokeza.
Viwango vya protini ijulikanayo kama Beta
Amyloid kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya
katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo hujenga
uchafu usiofutika kwenye ubongo na maradhi ya Alzheimer.
Majaribio yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha
Washington yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala kwa
dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na
uchafu panya hawa wakaanza kusinzia kwa dakika 30 pekee.

Ugonjwa wa sahau
Mmojapo wa wataalamu, Prof David Holtzman,
alisema: "endapo mapungufu katika usingizi huanza mapema kiasi hiki
katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa ishara ya
wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya."
"ikiwa matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi
hasa yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi kikamilifu au ni
tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu tofauti kabisa."
Hata hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia
panya mara nyingi hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi
zinazosababisha kutatizika na usingizi.
Dr Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea
Alzheimer's Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima
binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya kukosa usingizi
na ugonjwa wa Alzheimer.
Aliongezea kuwa: "tayari umekuwepo utafiti
unaounganisha mabadiliko katika usingizi huchangia katika matumizi ya
ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna uwezekano wa
kuwa mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara na onyo la
maradhi ya kusahau au Alzheimer.
Comments
Post a Comment