IRAN YAWAKOMALIA GOOGLE

Serikali ya Iran imebana huduma za mtandao wa tafuta tafuta wa Google,pamoja na huduma zake za barua pepe za Gmail.

Afisaa mmoja wa serikali amesema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kama tahadhari kufuatia maandamano makubwa ambayo yalikumba nchi za kiisilamu zilizokerwa na filamu ya Marekani iliyomkejeli Mtume Mohammad na dini ya kiisilamu.
Filamu hiyo ilipeperushwa kupitia mtando wa kijamii wa YouTube ambao unamilikiwa na Google.
Baadhi ya wanablogu, wamekemea hatua hiyo ya serikali kama inayolenga kukandamiza uhuru wa kujieleza
Maafisa wa utawala wamekuwa wakijiandaa kuzindua mtandao mwingine wa internet utakaotumika tu nchini humo ilinwananchi wakome kutumia mitandao ya kigeni.
Kwa mujibu wa maafisa wakuu, hatua hiyo italinda mtandao wa internet wa Iran kutokana na uvamizi kutoka nje.

Comments