Skip to main content
ULIPATA KUSIKIA ISUE YA JACQUELINE WOLPER KAMA BADO BASI MZIGO NDIO HUU..
Mcheza
filamu mkali wa hapa Bongo Jacqueline Wolper hivi karibuni alimshtua
mama’ake mzazi, wakiwemo wadau wa filamu baada ya kuonekana amelazwa
katika machela akiwa hoi taabani.
Tukio hilo ambalo lilikusanya watu wengi lilijiri Kibaha Mkoa wa Pwani ambako pia ndiko anakoishi mama mzazi wa staa huyo.
Watu
waliomzunguka yeye akiwa kitandani walisababisha waliokuwa wakipita
kufika eneo hilo kutaka kujua kulikoni, wengine walikwenda kumwambia
mama yake kuwa binti yake ameugua ghafla na kumfanya mwanamke huyo
kuchanganyikiwa.
Habari zikaendelea kudai kuwa, kufuatia hali hiyo, Mama Wolper
alimpigia simu mwanae kumuulizia kuhusu alichosikia, lakini akamjibu
haumwi yupo kazini.
Kwenye eneo la tukio, wakati watu wakiendelea kuulizana ndipo ilipogundulika kuwa staa huyo alikuwa akirekodi filamu.
Baadhi ya watu walionekana wakicheka baada ya kugundua kumbe kilichokuwa kikiendelea ni filamu na si tukio halisi.
“Yaani mimi niliogopa, nilijua labda amepata matatizo au anaumwa
ameletwa kwa mganga wa kienyeji,“ alisikika mtu mmoja akiwaambia wenzake
huku wakitawanyika eneo la tukio.
Comments
Post a Comment