DORTMUND NAYO YASHIKWA MBAVUNI

Eintracht Frankfurt's players salute the crowd after their 4-0 win at Hoffenheim in the BundesligaMabingwa watetezi wa Bundesliga 1, Borussia Dortmund, leo walibanwa mbavu na kutoka sare ya bao 1-1 ugenini na FC Nürnberg lakini Eintracht Frankfurt wameendeleza wimbi la ushindi na kupaa kileleni mwa Ligi hiyo baada ya kuifunga Hoffenheim bao 4-0.

Borussia Dortmund walianza Ligi Wiki iliyopita wakiwa nyumbani kwa kuifunga Werder Bremen lakini leo katika Mechi yao ya kwanza ugenini walijikuta wako nyuma kwa bao 1-0, kwa bao la Tomas Pekhart la Dakika ya 31 na Dakika 9 baadae Winga Jakub Blaszczykowski alisawazisha kwa Mabingwa hao.
Magwiji Bayern Munich wao wataingia dimbani kesho wakiwa nyumbani kucheza na VfB Stuttgart.
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Septemba 1
Bayer 04 Leverkusen 2 SC Freiburg 0
FC Nuremberg 1 BV Borussia Dortmund 1
Schalke 3 FC Augsburg 1
SV Werder Bremen 2 Hamburger SV 0
TSG Hoffenheim 0 Eintracht Frankfurt 4
Fortuna Dusseldorf v Borussia Mönchengladbach
Jumapili Septemba 2
VfL Wolfsburgv Hannover 96

Comments