CHINA YAMPELEKA KIZIMBANI MKUU WA JESHI LA POLISI MSTAAFU

Kesi ya siku mbili ya mkuu wa zamani wa polisi wa uchina kuhusiana na kashfa ya kisiasa imeanza nchini humo
Wang Lijun anashutumiwa kwa makosa ya utoro kazini na kujaribu kuficha mauaji ya mfanyabiashara wa kiingereza aliyeuawa Kusini Magharibi mwa mji wa Chengdu.
Hukumu dhidi yake inatarajiwa kutolewa muda mfupi ujao . Bwana Wang alijisalimisha kwa maafisa wa usalama mwezi Machi baada ya kutafuta hifadhi kwenye ubalozi mdogo wa Marekani mjini Chengdu.
Alitoa shutuma zilizosababisha kufutwa kazi kwa mkuu wake , Bo Xilai, ambaye amekuwa mmoja wa viongozi wa Uchina wanao nawiri kisiasa.
Mkewe bwana Bo , Gu Kailai, baadaye alipatikana na hatia ya kumuua mfanyabiashara wa Uingereza Neil Heywood

Comments