CHELSEA ACHEZEA KICHAPO HUKO MONACO

  --  FALCAO ajithibisha kama anauwezo wa ajabu.
Jana huko Monaco Stade Louis II, Mabingwa wa EUROPA LIGI, Atletico Madrid, wamewachapa Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, kwa bao 4-1, Bao 3 zikiwa toka kwa Straika wao hatari Falcao, na kutwaa UEFA SUPER CUP.

Katika Mechi hii, Atletico Madrid walionyesha wako hatari na wepesi sana wakinasa mpira na kuanza mashambulizi ya haraka, 'kaunta ataki', ambazo kila mara zilionyesha udhaifu mkubwa wa Difensi ya Chelsea iliyokosa umoja na mbinu za kuwakabili Atletico.
Leo Mtu 4 za Difensi ya Chelsea walikuwa ni Ivanovic, Cahill, Luiz na Cole.
Hadi mapumziko, Atletico walikuwa mbele kwa Bao 3 za Falcao.
Kipindi cha Pili, Chelsea walipata Bao lao moja alilofunga Sentahafu wao Gary Cahill kufuatia patashika baada ya kona.
VIKOSI:
ATLETICO MARID: Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis, Mario Suarez, Gabi, Adrian, Koke, Turan, Falcao.
Akiba: Sergio Asenjo, Raul Garcia, Rodriguez, Silvio, Cata Diaz, Diego Costa, Emre.
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Mikel, Lampard, Ramires, Hazard, Mata, Torres.
Akiba: Turnbull, Romeu, Oscar, Moses, Meireles, Sturridge, Bertrand.
Refa: Damir Skomina (Slovenia)
 
Wafungaji Magoli
Atletico
-Falcao=6, 19 na 45
-Miranda=60
Chelsea
-Gary Cahill=75

Comments