
"Alizungumza vyema, anaonekana kuwa mwenye afya nzuri, na angelipenda kwa mara nyingine kushangiliwa."
Hatton, ambaye alibandikwa jina la utani 'The Hitman', yaani 'mgongaji', hajawahi kupigana tena tangu aliposhindwa kwa KO katika raundi ya pili, alipotandikana na Manny Pacquiao mwezi Mei, mwaka 2009.
Mwaka 2010, bodi hiyo ya ngumi ilimpokonya Hatton leseni, kufuatia madai ya kutumia dawa ya kulevya ya cocaine.
"Anaonekana yuko katika hali nzuri kabisa, hana shida yoyote, na inaelekea hana matatizo yoyote," alielezea Smith.
"Kutokana na matamshi yake, inaelekea ametulia vyema na familia yake. Tayari ameshapitia ukaguzi fulani wa kimatibabu, na tumo katika kuhakikisha anakamilisha utaratibu mzima."
Comments
Post a Comment