Skip to main content
BILL CLINTON HAMNUSURU RAS OBAMA..
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton amemtetea vikali mgombea urais wa chama cha Democrats nchini Marekani Barack Obama.Katika hotuba iliyochukua muda wa dakika 50 katika kongamano la chama
hicho linalofanyika mjini Charlotte, North Carolina, Clinton alikosoa
sera za uchumi za chama pinzani cha Republican.
Bill alisisitiza kuwa sera ya uchumi
ya Barack Obama imeweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo ambao ulikuwa
umedorora. Bwana Clinton alimaliza hotuba yake kwa kumteua rais Obama
kuwa mgombea rasmi wa urais wa chama.
Rais Obama atamenyana na mgombea wa chama cha Republican Mitt Romney katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba.
Hotuba ya Clinton ni dalili ya kuimarika kwa
uhusiano kati yake na Obama na pia kama juhudi za kupiga jeki mvuto wa
obama miongoni mwa wazungu wanaofanya kazi.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa wapiga kura wa
chama hicho wamekuwa waangalifu sana kuhusu sera za Obama lakini Clinton
ana rekodi nzuri ya kuwashawishi watu kumuunga mkono Obama.
Clinton aliambia wafuasi wa chama '' Amueni nchi
mnayotaka kuishi. Ikiwa mnataka viongozi wasio wajali basi pigieni kura
chama cha Republican. Mkitaka nchi yenye nafasi nyingi na ambayo
majukumu yanagawanywa, basi sote tuko pamoja. Lazima mumpigie kura
Barack Obama na makamu wake Joe Biden."
Bwana Clinton alikosoa vikali chama cha
republican kwa kuzuia juhudi za uchepuzi wa uchumi na badala yake
kujihusisha na mijadala kuhusu sera.
Kura za maoni zinaonyesha Barack Obama akiongoza
kwa asilimia 47 huku mpinzani wake Mit Romney akimfuata kwa asilimia
arobaini na sita.
Comments
Post a Comment