ALIYEKUWA MKUU WA POLISI CHINA AHUKUMIWA MIAKA 15 GEREZANI

Aliyekuwa mkuu wa polisi Uchina anayeandamwa na kashfa ya kisiasa amehukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani katika kesi itakayosaidia kuamua hatima ya aliyekuwa mkuu wake Bo Xilai.

Wang Lijun alikiri makosa ya kuasi, kutumia vibaya mamlaka na kujaribu kuficha mauaji ya mfanya biashara mmoja Muingereza.
Waandishi wanasema Wang Lijun ameonewa huruma kwa kufichuwa mauaji hayo ambayo baadaye mkewe Bo Xilai alihukumiwa.
Bo Xilai amepokonywa mamlaka katika chama cha kikomyunisti lakini haijabainika iwapo atashtakiwa kwa makosa ya uhalifu.
Vyombo vya habari vya kitaifa viliripoti kuwa Bo alimshambulia Wang Lijun alipofichua kwamba mkewe alihusika katika mauaji hayo.

Comments