Akizungumza na mtandao huu eneo la soko hilo, Ofisa Uhusiano wa Chuo cha Kijeshi cha Pangawe, Meja Andrew Komba, alisema wameamua kufanya hivyo ikiwa ni njia mojawapo wa kuadhimisha sherehe hizo. "Kabla ya kufika hapa tulitembelea kituo cha watoto yatima cha Mgolole, Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako tuliwapa pole wagonjwa na baadaye tuliamua kuja hapa sokoni kufanya usafi wa soko, ndani na nje," alisema Meja Komba.
Comments
Post a Comment