Mechi za Mashindano makubwa ya Klabu
Barani Afrika, CHAMPIONZ LIGI na Kombe la Shirikisho, yanaendelea
Wikiendi hii kwa Mechi za Makundi huku Kundi A la CHAMPIONZ LIGI likiwa
tayari limepata wawakilishi wawili watakaocheza Nusu Fainali baada ya
kufutwa kwenye Mashindano na CAF kwa Klabu ya Tunisia, ES Sahel.
Timu zilizofuzu toka Kundi A ni Mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia na Sunshine Stars ya Nigeria.
Kundi B bado lina utata lakini Al Ahly
yupo kileleni akiwa na Pointi 10 na ana nafasi nzuri ya kufuzu na nyuma
yao wako TP Mazembe ya Congo DR, wenye Pointi 7, na Bechem Chelsea,
ambao wana Pointi 5.
Mechi ambayo itaamua nini mustakabali wa
Kundi hili ni ile ya Jumapili huko Stade Frederic Kibassa Maliba,
Lubumbashi ambako Wenyeji TP Mazembe, wakiwa na Straika hatari wa
Tanzania Mbwaba Samatta, watakapoikaribisha Al Ahly.
RATIBA YAMICHUANO YA KLABUBINGWA BARANI AFRICA
[Kwenye Mabano matokeo Mechi ya kwanza]
Jumamosi Septemba 1
[Saa 3 Usiku]
Al Zamalek – Egypt v Bechem Chelsea – Ghana [2-3]
Jumapili Septemba 2
[Saa 10 na Nusu Jioni]
TP Mazembe - Congo, DR v Al Ahly – Egypt [1-2]
[Saa 4 na Nusu Usiku]
EspĂ©rance Sportive de Tunis – Tunisia V Sunshine Stars – Nigeria [2-0]
================
MSIMAMO=CHAMPIONZ LIGI:
KUNDI A
1 Esperance Mechi 2 Pointi 6==Imeingia Nusu Fainali
2 Sunshine Stars Mechi 3 Pointi 6==Imeingia Nusu Fainali
3 ASO Chlef Mechi 3 Pointi 0
FAHAMU: ES Sahel ya Tunisia imeondolewa kwenye Mashindano na CAF
KUNDI B
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Al Ahly Pointi 10
2 TP Mazembe 7
3 Bechem Chelsea 5
4 Al Zamalek 0
FAHAMU: Timu mbili za juu zinaingia Nusu Fainali.
================
RATIBA-KOMBE LA SHIRIKISHO
Ijumaa Agosti 31
El Merreikh [Sudan] v Ahli Shandi [Sudan]
Jumamosi Septemba 1
GD Interclube [Angola] v Al-Hilal [Sudan]
Stade Malien de Bamako [Mali] v AC Leopards de Dolisie [Congo]
Jumapili Septemba 2
Djoliba AC [Mali] v Wydad Athletic Club [Morocco]
================
MSIMAMO=KOMBE LA SHIRIKISHO
KUNDI A
1 El Hilal Pointi 4
2 El Merreikh 4 3
3 El Ahly Shandy
4 InterClube 0
KUNDI B
1 Djoliba Pointi 4
2 AC Léopards 2
3 Wydad Casablanca 2
4 Stade Malien 1
================
Comments
Post a Comment