HUYU NDIE MAMA DIAMOND PLATNUM..

 
SIRI imefichuka! Kumbe mwanamuziki ‘anaye-hit’ kwa sasa katika muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platinumz’ na mama yake mzazi, Sanura Khassim ‘Sandra’ walianza kupendana zamani, Amani linashuka nayo.

 Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya familia hiyo, Sandra ndiye aliyemlea Diamond na kupita katika vipindi vigumu kimaisha baada ya baba yake, Abdul Jumaa kutengana na mama yake ndiyo maana mara nyingi huwa wanaambatana hata kwenye shoo za msanii huyo ambazo kuna uwezekano wa mzazi huyo kuhudhuria.

“Sandra ndiye aliyemsomesha Diamond kwa shida hivyo hawezi kuacha kumpenda na ndio maana kila sehemu akiambiwa hawashukuru watu waliomfanya afike hapa alipo wa kwanza kumtaja ni Mama yake kilisema chanzo hicho..We msikilize Diamond akiwa anahojiwaa ataanza kumshukuru Mungu Then Mama yake pia chanzo hiko kimethibitisha kuwa Diamond mda mwingine anasahau suala la kuoa kwa sababu ya upendo tosha anaoupata kutoka kwa Mama yake,Hata Mama yake pia ndio maana hataki kuolewa kwasababu kuna mtu anaependa kw dhati ambaye ni Diamond Mwanae, Kwa mujibu wa Diamond mwenyewe wakati anaangaikia suara la kutoka kimuziki mamaake ndie akiemuangaikia na kumpeleka kwenye Talent show mbarimbari, Kwahiyo ni dhahili kuwa Mama Diamond ndie alietoa mchango mkubwa kwa Diamond.



Comments