HODGSON ATANGAZA KIKOSI CHA ENGLAND CHA KOMBE LA DUNIA.

 
   TERRY Akabiziwa kazi nzito
Nahodha wa Chelsea John Terry ametajwa kwenye Kikosi cha England ambacho kitacheza Mechi za Kundi


 kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil dhidi ya Moldova na Ukraine licha ya kukabiliwa na Kesi ya Chama cha Soka England, FA, ya kumkashifu kibaguzi Sentahafu wa QPR Anton Ferdinand lakini Winga wa Manchester United Ashley Young hakuchukuliwa.

Kwenye Kombe la Dunia Kanda ya Ulaya, England wapo Kundi H na watacheza ugenini na Moldova hapo Septemba 7 na Septemba 11 watakuwa kwao Uwanja wa Wembley Jijini London kucheza na Ukraine.
Timu nyingine kwenye Kundi H ni Poland, Montenegro na San Marino.
Nae Kiungo wa Manchester United, Michael Carrick, ameitwa tena baada ya kumaliza mgomo wake wa kutoichezea England lakini alicheza Mechi ya mwisho walipocheza na Italy mapema Mwezi huu.
Majeruhi Wayne Rooney hayumo na badala yake wapo Mastraika wanne kina Andy Carroll, Jermain Defoe, Daniel Sturridge na Danny Welbeck.
Kwa kumtema Young, Kocha Roy Hodgson amewachukua Mawinga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Theo Walcott pamoja na James Milner wa Manchester City na Adam Johnson wa Sunderland.
KIKOSI KAMILI:
Makipa: Jack Butland (Birmingham City), Joe Hart (Manchester City), John Ruddy (Norwich City).
Mabeki: Leighton Baines (Everton), Ryan Bertrand (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Joleon Lescott (Manchester City), John Terry (Chelsea), Kyle Walker (Tottenham Hotspur).
Viungo: Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley (Manchester United), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Johnson (Sunderland), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Theo Walcott (Arsenal).
Mafowadi: Andy Carroll (Liverpool), Jermain Defoe (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Chelsea), Danny Welbeck (Manchester United).

Comments