
Miaka 14 iliyopita, katika Mechi ya
kwanza ya UEFA SUPER CUP kuchezwa ndani ya Stade Louis II, Monaco,
Kiungo wa Chelsea alikuwa Roberto Di Matteo na walitwaa Kombe hilo kwa
kuifunga Real Madrid Bao 1-0 na leo hii, Roberto Di Matteo, anaiongoza
Chelsea kama Meneja wake akiwania kutwaa tena Taji hilo ambalo
linashindaniwa Stade Louis II kwa mara ya mwisho.
UEFA SUPER CUP hushindaniwa kila Mwaka,
kabla tu ya hatua za Makundi za CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI kuchezwa,
na hugombewa na Bingwa wa CHAMPIONZ LIGI, safari hii ni Chelsea, na
Bingwa wa EUROPA LIGI, ambae mara hii ni Atletico Madrid.

Di Matteo ameahidi kulibeba Kombe na kulirudisha Stamford Bridge.
Msimu huu, Chelsea kama vile wapinzani
wao Atletico Madrid, wameuanza vizuri kwa ushindi kwenye Ligi zao lakini
Di Matteo amesema: “Nafurahi na mwanzo mzuri na jinsi Wachezaji
wanavyocheza. Lakini bado kuna haja ya kujiboresha zaidi.”
Atletico wao walitwaa UEFA SUPER CUP
Miaka miwili iliyopita lakini Kocha wao Diego Simeone amesema Chelsea
ndio wenye nafasi kubwa kushinda.
Hata hivyo, historia ya UEFA SUPER CUP
inaonyesha tangu Mwaka 2000 ni Timu 5 tu kati ya 12 zilizotwaa UEFA
CHAMPIONZ LIGI ndio zimefanikiwa kutwaa Kombe hili.
Wachezaji

Torres, Mika 28, alijizolea sifa akiwa na Atletico ambako aliifungia Bao 82.
Nahodha wa Chelsea, John Terry, ataikosa
Mechi hii kwa vile yupo kifungoni kufuatia kutolewa kwake kwa Kadi
Nyekundu wakati Chelsea ilipocheza na Barcelona Msimu uliopita na
mbadala wake anaweza kuwa Mbrazil David Luis.
Tegemezi kubwa la Atletico ni Straika wao hatari Falcao ambae ndie mashine yao ya magoli.
Comments
Post a Comment